Monday, February 04, 2013

NHC yakabidhi mabati 1,000 kwajili ya ujenzi wa mabweni ya shule za sekondari za wasichana


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rose Lulabuka (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kukabidhiwa rasmi mabati 1,000 yenye thamani ya Sh 20 milioni yaliyotolewa kama msaada na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Umma (NHC) , Susan Omari na kulia kabisa ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa wilaya ya Kongwa. Mabati hayo yatatumika kuezekea mabweni ya shule ya sekondari za wasichana Kibaigwa, mkoani Dodoma. (Picha kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rose Lulabuka (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya mabati 1,000 yenye thamani ya Sh 20 milioni yaliyotolewa kama msaada na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Umma (NHC) , Susan Omari (k. Mabati hayo yatatumika kuezekea mabweni ya shule ya sekondari za wasichana Kibaigwa, mkoani Dodoma. (Picha kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)

No comments: